NDEMLA KWENDA KUJARIBU ‘ZALI’ SWEDEN KESHO

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Manara inasema kiungo Said Ndemla ataondoka kesho kuelekea nchini Sweden kufanya majaribio ya wiki mbili katika klabu ya AFC Eskilstuna.

Timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo pia anachezea Mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ambapo majaribio hayo ya Ndemla ni ishara nzuri kwa nyota wengine wa hapa nchini.

Ndemla anafahamika vizuri kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti atafanya majaribio ya siku 14 na endapo atafaulu Eskilstuna itakaa mezani na Simba kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Kama kiungo huyo atafanikiwa kufaulu majaribio hayo Ndemla ataongeza idadi ya wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Ndemla ataungana na Mbwana Samata, Ulimwengu na Farid Musa wanaocheza soka barani Ulaya.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *