NEWCASTLE YAIDUWAZA ARSENAL ST JAMES PARK

Washika bunduki wa London timu ya Arsenal wamekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Newcastle United katika mchezo wa ligi kuu Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa St James Park.

Arsenal ilimiliki mpira kama kawaida yao lakini hawakuwa na madhara katika lango la Newcastle kwani wenyeji hao walikuwa makini kuondoa hatari zote.

Mshambuliaji Alexander Lacazzate aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 14 baada ya kupokea pasi ya Pierre Aubameyang.

Newcastle ilisawazisha bao hilo dakika ya 29 kupitia kwa Ayoze Perez kabla ya Matt Ritchie kuongeza la pili dakika ya 68.

Newcastle imefikisha pointi 41 ikiwa nafasi ya 10 wakati Arsenal imebaki nafasi ya sita ikiwa na alama zake 54.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *