NEYMAR: Chicharito ukiwafunga United shangilia tu

BAADA ya straika mpya wa West Ham United, Javier Hernandez ‘Chicharito’ kushindwa kuweka wazi kama atashangilia au la endapo ataifunga timu yake ya zamani, Manchester United, Neymar ameuponda utamaduni huo.

United watawakaribisha ‘Hammers’ jioni ya leo kwenye uwanja wa Old Trafford katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza.

Chicharito aliulizwa na wanahabari kuhusu kitakachotokea endapo ataifunga United ndipo alipopata wakati mgumu kuwa muwazi.

Javier Hernandez ‘Chicharito’

“Sijui kama nitashangilia nikifunga bao pale, ni timu yangu ya zamani, ni mashabiki wangu wa zamani, ni uwanja wangu wa zamani lakini itakuwa ni bao langu la kwanza katika timu yangu mpya.

“Sifikirii kuhusu kushangilia, nataka kuanza na kuipa matokeo timu yangu, mimi ni mchezaji wa West Ham, nataka kufanya vizuri hapa zaidi ya nilivyofanya United,” alisema Chicharito.

Nyota mpya wa PSG, Neymar amekuwa na mtazamo tofauti kuhusiana na jambo hilo huku yeye akisema kutoshangilia mabao dhidi ya timu za zamani ni utamaduni wa ajabu.

Neymar

“Kufunga bao kunaleta hisia nzuri sana, liwe la ushindi, la kusawazisha, dhidi ya wapinzani wa jadi, bao pekee katika ushindi au linaloamua matokeo.

“Kutoshangilia bao iwe dhidi ya timu yako ya zamani au vinginevyo ni utamaduni mbovu kabisa,” alisema Neymar akimaanisha siku akikutana na Barcelona na akafunga bao atashangilia kwa nguvu zote.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *