NEYMAR: UEFA ifungieni Barcelona.

NEYMAR,amekiomba chama cha mpira wa miguu barani Ulaya “UEFA” kuifungia klabu ya Barcelona kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kushindwa kumlipa “Bonas” yake ya paundi milioni 23.

Neymar amefikia hatua hiyo kufuatia ushauri aliopewa na wanasheria wake wa kuichukulia klabu yake ya zamani hatua kali kwa kushindwa kutoa kiasi hicho cha pesa baada ya yeye kusajili PSG jambo lililosababisha moja ya wakuregenzi bw.Raul Sanllehi kuachia ngazi.

kwa mujibu wa mtandao wa AS wa nchini hispania, UEFA imelitupilia mbali ombi hilo, hivyo Barcelona haitatolewa katika michuano hiyo kama Neymar alivyoomba.

Usajili wa Neymar ulivutwa mpaka mwezi Agosti kwa makusudi ili baba yake mzazi aweze kupokea kiasi hicho cha pesa mwishoni mwa mwezi julai, jambo ambalo klabu ya Barcelona ililikataa kwa kudai mchezaji huyo amekiuka masharti ya kimkataba kwa kufanya makubalioano na klabu ya PSG kabla ya muda huo.

Neymar amekua na mwanzo mzuri na klabu yake mpya iliyomsajili kwa dau lililovunja rekodi ya dunia akiwa ameshaifungia mabao 8 katika michezo 8 ambayo amecheza.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *