Ngoma Akata Mzizi wa Fitina

MSHAMBULIAJI Donald Ngoma wa Yanga amefuta uvumi wa kutaka kutimka klabuni hapo baada ya kusaini mkataba wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa ligi mara tatu mfululizo.

Jana mtandao wa KickOff.com wa Afrika Kusini ulitoa taarifa kuwa raia huyo wa Zimbabwe amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu ya Polokwane City ya nchini humo kabla ya uongozi wa Yanga kukanusha taarifa hiyo.

Mchana huu kumetoka picha zikimuonyesha mshambuliaji huyo akisaini mkataba mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya klabu hiyo Hussein Nyika wa kuendelea kubaki kwa mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu.

Katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa alishindwa kuuthibitisha mtandao huu moja kwa moja kuwa mshambuliaji huyo amesaini mkataba mpya akisema kama picha zimeonekana kwenye mitandao itakuwa ni kweli kwakua walikuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kumalizia dili hilo.

“Suala la usajili lipo chini ya kamati siwezi kuliingilia, kama umeona picha kwenye mitandao zikimuonyesha Ngoma anasaini itakuwa kweli kwakua walikuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili hilo toka asubuhi,” alisema Mkwasa.

Taarifa hii ni njema kwa mashabiki wa mabingwa hao baada ya wiki mbili zilizopita kutangaza kuachana na kiungo wao fundi Haruna Niyonzima baada ya kushindwana katika masuala ya maslahi hivyo kusaini kwa mshambuliaji huyo kutaendeleza imani ya kufanya vizuri msimu ujao wa ligi kutokana na umuhimu wake kikosini.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *