NGOMA BADO KIDOGO MPAKA DISEMBA 28

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma ataendelea kusubiri kwa wiki mbili ili awe fiti asilimia mia kabla ya kurejea uwanjani.

Ngoma amekuwa akiandamwa na majeruhi ya muda mrefu katika kipindi hiki akiwa amecheza mechi chache za mwanzoni mwa msimu ambapo hajarudi tena dimbani mpaka sasa.

Msemaji wa timu hiyo Dismas Ten amesema kuwa mshambuliaji huyo anaendelea vizuri lakini Daktari amemtaka kukaa nje kwa wiki mbili zaidi ili kupona kabisa.

“Ngoma atarejea uwanjani Disemba 28 kwa mujibu wa taarifa ya Daktari ingawa hali yake inaendelea vizuri inatakiwa apone kabisa,” alisema Ten.

Kurejea kwa raia huyo wa Zimbabwe kunawafanya mabingwa hao watetezi wa ligi kubaki na Thaban Kamusoko na Kelvin Yondani ambaye nae atarejea baada ya wiki mbili.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *