NGOMA NJE HADI AGOSTI 11

Mshambuliaji mpya wa Azam FC raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma atakuwa nje ya uwanja hadi Agosti 11 kwa mujibu wa vipimo alivyofanyiwa katika hospitali ya St Vincent Parrot ya Afrika Kusini.

Ngoma aliondoka nchini wiki moja iliyopita kuelekea Afrika Kusini akiwa sambamba na daktari wa timu hiyo Mwanandi Mwankemwa na wamerejea leo saa 3 asubuhi.

Dk Mwankemwa amethibitisha kuwa Ngoma atakuwa nje ya hadi Agosti 11 kwa ajili ya kuuguza goti lake ambalo lina uvimbe.

Mwankemwa amesema Ngoma ana uvimbe kwenye goti la kulia ambapo baada ya vipimo imeonekana alikuwa amechanika kidogo japo tayari ameanza kupona.

Hata hivyo dokta huyo aliongeza kuwa Ngoma hatafanyiwa upasuaji badala yake ataendelea kufanya mazoezi mepesi ya kawaida mwenyewe kabla ya kupona kabisa na kurejea uwanjani.

“Vipimo alivyofanyiwa Ngoma vinaonyesha atakaa nje ya uwanja kwa wiki tisa ili kupona kabisa ambapo itakuwa hadi mwezi wa Agosti,” alisema Dk. Mwankemwa.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *