NI RONALDO TENA, ACHUKUA BALLON D’OR YA TANO KAMA MESSI

Cristiano Ronaldo amemfikia Lionel Messi kwa kuweka rekodi ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or mara tano katika tuzo zilizofanyika jijini Paris.

Ronaldo aliiongoza Real Madrid kutwaa ligi ya mabingwa mara 12 mwezi Juni huku akifunga hat-trick dhidi ya Bayern Munich na Atletico Madrid katika hatua ya nusu fainali pia alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa fainali walioshinda mabao 4-1 dhidi ya Juventus.

Messi ambaye hivi karibuni alisaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Barcelona amekamata nafasi ya pili kwa mara ya pili mfululizo.

Mchezaji ghali wa duniani kwa sasa ameshika nafasi ya tatu kwa mara ya pili katika miaka mitatu.

Kiungo N’Golo Kante ameshika nafasi ya nane na ndio kinara kwa ligi kuu ya Uingereza huku Harry Kane akikamata nafasi ya 10.

Kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne ameshika nafasi ya 14 wakati Eden Hazard wa Chelsea akikamata nafasi ya 19 huku mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea akiwa wa 20

Sadio Mane wa Liverpool amekamata nafasi ya 23 huku Philippe Coutinho akiwa wa 29.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *