NUSU FAINALI KAGAME CUP KUPIGWA KESHO SAA 8 MCHANA

Mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Kagame Cup baina ya Azam FC dhidi ya Gor Mahia utafanyika kesho saa 8 mchana katika uwanja wa Taifa.

Nusu fainali ya pili baina ya Simba na JKU itaanza saa 11 jioni katika uwanja huo huo wa Taifa.

Katibu mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye amesema wameamua kupanga muda huo ili kutoingiliana na ratiba ya kombe la dunia ambapo mashabiki watakuwa na nafasi ya kufuatilia mashindano hayo baada ya mechi za Kagame.

“Tunafahamu kesho kutakuwa na mechi za nusu fainali ya kombe la dunia usiku sisi tunafanya mechi zetu mapema ili kutoa nafasi kwa mashabiki kufuatilia,” alisema Musonye.

Gor Mahia ndio timu pekee kutoka nje ya Tanzania ambayo imetinga hatua hiyo ambayo imepangwa kucheza na bingwa mtetezi Azam.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *