Nyota Madrid ‘wamchoka’ Bale

NYOTA wa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, Isco na Marco Asensio wamechoshwa na mchango mdogo wa Gareth Bale klabuni hapo tangu kuanza kwa msimu huu.

Madrid wamedroo michezo miwili kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu dhidi ya Valencia na Levante na kwa mujibu wa gazeti la Don Balon la nchini Hispania, wachezaji wa timu hiyo wameanza kucharukiana kutokana na matokeo hayo mabovu.

Taarifa zinasema Isco na Asensio wamechoshwa na ubinafsi wake uwanjani ambao hauisaidii timu huku wakishangazwa na kocha Zidane kuendelea kumng’ang’ania kwenye kikosi cha kwanza.

Licha ya kiwango bora cha Isco mwaka huu huku Asensio akitupia mabao manne katika mechi tano chini ya Zidane, wawili hao wamekuwa hawana uhakika katika kikosi cha kwanza ingawa kwasasa Asensio anacheza kutokana na kukosekana kwa Cristiano Ronaldo.

Mabingwa hao watetezi wamejikuta wapo nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga baada ya kucheza mechi tatu huku mahasimu wao Barcelona wakiwa kileleni kwa kushinda mechi zote tena bila kuruhusu hata bao moja.

Madrid watashuka dimbani usiku wa Jumatano hii dhidi ya Apoel katika kampeni za kutetea tena taji lao la ligi ya mabingwa Ulaya.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *