Nyota Sunderland Aanzisha Timu Jela

YORKSHIRE, Uingereza
ALIYEKUWA mshambuliaji wa Sunderland Adam Johson 29, aliyehukumiwa miaka sita jela kufuatia kukutwa na hatia ya kujihusisha kimapenzi na binti aliye chini ya miaka 18 ameanzisha timu ya mpira wa miguu akiwa gerezani.

Nyota huyo ameanzisha timu akiita ‘Johson Superstars’ akiwa kiongozi wa wafungwa wenzake ndani ya gereza la HMP Moorland alipofungwa.

Johnson alijihusisha kimapenzi na binti wa miaka 15 na kufanya bao lake dhidi ya Liverpool katika matokeo ya 2-2 kuwa la mwisho katika maisha yake ya soka kabla hajaingia kifungoni.

nintchdbpict000222951066-e1486563773491

Johnson huwapa mazoezi ya dakika 15 wafungwa wenzake katika timu yake kabla hawajacheza mechi dhidi ya wapinzani wanaokutana nao katika viwanja mbalimbali vya wafungwa.

Taarifa kutoka chanzo ndani ya gereza hilo inasema Johnson anaishi gerezani bila kuwa na hofu yoyote bali anafurahia maisha kila siku kutokana na jinsi anavyoishi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *