Okwi aanza yake Simba ikiituliza Mtibwa

MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi ameanza vitu vyake baada ya kuiwezesha timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa bao moja katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Okwi alifunga bao hilo dakika ya 45 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na John Bocco kuwahadaa mabeki wa Mtibwa kufuatia pasi aliyopewa na Shiza Kichuya.

Emmanuel Okwi

Simba walianza mchezo huo taratibu ambapo walicheza zaidi katika eneo la katikati ya uwanja huku mlinda mlango Said Mohammed ‘Nduda’ akiokoa michomo miwili iliyokuwa ikielekea kimiani.

Simba walirudi kwa kasi kipindi cha pili kwa kuliandama lango la Mtibwa huku kiungo mpya Haruna Niyonzima akitoa burudani ya ‘bure’ kwa mashabiki waliohudhuria kwa chenga za maudhi na pasi za malengo.

Niyonzima akiwatoka nyota wa Mtibwa

Wekundu hao walitengeza nafasi nyingi za kufunga hasa kipindi cha pili lakini safu yao ya ushambuliaji ilikosa umakini na utulivu ikifika katika lango la Mtibwa.

Kikosi cha Simba kitaondoka kesho kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya siku 10 kabla ya kukutana na watani wao wa jadi Yanga Agosti 23.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *