Okwi amjeruhi Omog mazoezini

WINGA wa kimataifa wa Simba raia wa Uganda Emmanuel Okwi leo amegongana na kocha wa timu hiyo Joseph Omog na kumsababishia jeraha juu ya jicho wakiwa mazoezini kwenye uwanja wa Uhuru.

Omog alikuwa akifundisha mbinu ya kushambulia kwa kutumia walinzi wa pembeni kisha mawinga kuingia ndani kwa kasi kumalizia krosi za mabeki hao.

Tukio hilo lilitokea wakati Okwi akikimbia kwa kasi kuiwahi krosi katika eneo la karibu na lango ambapo kocha Omog alikuwa amesimama kabla hawajagongana.

Kocha Omog baada ya kupatiwa matibabu

Daktari wa wekundu hao, Yassin Gembe alilazimika kumfunga bandeji kocha huyo na kumpumzisha kwa dakika kadhaa kabla hajarejea uwanjani kuendelea na majukumu yake.

Kwa upande wake Okwi yeye hakudhurika sana, alitibiwa hapo hapo uwanjani na kuendelea na mazoezi.

Simba inajiandaa na pambano la tatu la ligi kuu dhidi ya Mwadui FC litakalopigwa Jumamosi ijayo katika dimba hilo hilo la Uhuru.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *