OKWI, KAGERE WAING’ARISHA SIMBA UTURUKI

Safu ya ushambuliaji ya timu ya Simba imeonyesha makucha yake baada ya kuichapa F.C.E Ksaifa ya Palestina mabao 3-1 katika mchezo wa pili wa kirafiki uliofanyika nchini Uturuki.

Mshambuliaji Emmanuel Okwi aliifunga mabao dakika za 16 na 50 kabla ya kufanyiwa mabadiliko.

Meddie Kagere aliyetokea benchi alikamilisha karamu hiyo ya mabao kwa kufunga la tatu dakika ya 87 na kutuma salamu kuwa msimu huu wana safu imara ya ushambuliaji.

Bao pekee la Wapalestina hao lilifungwa dakika ya 54 na Nader Alkrinaui.

Katika mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Moulodia Oudja uliomalizika dakika ya 65 kutokana na mvua kubwa kuonyesha timu hizo zilitoka sare ya bao moja huku la Simba likifungwa na Adam Salamba.

Simba inatarajia kurejea nchini alfajiri ya Jumatatu kutoka Uturuki kwa ajili ya tamasha la Simba Day, Agosti 8 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *