OKWI: Natamani niwe na mpira muda wote

WINGA wa wekundu wa Msimbazi Simba, Emmanuel Okwi amesema licha ya kuwa ni ajira yake, mpira wa miguu unabakia kuwa mchezo anaoupenda kuliko yote duniani.

Akizungumza na mwandishi wa Simba Makini baada ya mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Boko Veterans, Okwi alisema tangu ajitambue soka imekuwa sehemu ya maisha yake huku akikiri kuna wakati anatamani hata kulala na mpira  kitandani.

“Mpira ni kazi yangu, lakini hata nisingekuwa na kipaji naamini bado ningeupenda, huwa natamani kila muda niwe na mpira jirani yangu,” alisema Okwi.

Wakati mazoezi yakiendelea na hata baada ya kumalizika Okwi alionekana akiwa na mipira mitatu hadi minne kwa wakati mmoja hali iliyomfanya mwandishi wetu atake kujua sababu.

Okwi akiwa na mipira mitatu

Winga huyo ambaye alikiri kutamani mpira hata akiwa uwanjani kwenye mechi, ataiongoza safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports kwenye tamasha la Simba Day.

Hizi hapa ni baadhi ya picha za mazoezi ya leo.

Niyonzima kushoto akijadili jambo na kipa Said Mohamed ‘Nduda’
Huyu ndiye Nicholas Gyan, anatarajiwa kuibeba Simba kwenye safu ya ushambuliaji
Mohamed Ibrahim, Said Ndemla na James Kotei ni baadhi ya viungo wa Simba

 

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *