Okwi Sasa Rasmi Simba

WINGA wa Uganda Emmanuel Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kuanzia msimu ujao.

Okwi ambaye anarejea kwa mara nyingine Msimbazi ataichezea timu hiyo katika michuano yote ikiwemo ligi kuu ya Vodacom, FA na kombe la shirikisho barani Afrika.

Akizungumza katika utiaji saini mkataba huo, mwanachama maarufu wa Simba bilionea Mohamed Dewji ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwa klabu alisema Okwi ni zawadi ya Eid kwa wanasimba.

“Nawatakia sikukuu njema wanasimba wote na naomba nitoe zawadi kwao ambayo ni Okwi, karibu sana Simba Okwi,” alisema Dewji.

Tangu arejee kutoka nchini Denmark na kujiunga na SC Villa, Okwi amekuwa katika kiwango bora kilichopelekea arejeshwe timu ya taifa ‘The Cranes’ hivyo kuashiria Simba wamelamba ‘dume’ katika usajili huo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *