OKWI: Ushindi umetupatia mzuka wa kuanza ligi

MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi wa Simba amesema ushindi wa ngao ya jamii walioupata jana dhidi ya Yanga umewaongezea morali ya kuanza vyema msimu mpya wa ligi kuu wikiendi ijayo.

Okwi ambaye ni mmoja wa wachezaji wa Simba wanaopendwa sana na mashabiki wa Wekundu hao amesema ushindi huo utawafanya kuanza ligi bila presha kuliko kama wangepoteza mtanange huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa.

Simba ambayo imefanya usajili mkubwa msimu huu ilikuwa ikipewa nafasi ya kushinda katika mchezo kirahisi lakini Yanga walifanya kazi kubwa kuwadhibiti Wekundu hao hali iliyopelekea mechi kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.

“Hii ni ishara nzuri kuelekea kuanza ligi wikiendi ijayo, ushindi wa jana utatufanya kuanza ligi bila presha na matumaini yangu tutaanza vizuri,” alisema Okwi.

Simba itaanza na Ruvu Shooting katika mechi ya kwanza keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo wa jana Simba ilishinda kwa penati 5-4 baada ya kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *