Owen aipa ubingwa Chelsea

LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Liverpool, Michael Owen amesema Chelsea ina nafasi kubwa ya kutetea taji la ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao huku timu za Manchester United na Liverpool zikiwa ndio wapinzani wakuu.

Licha ya timu hiyo kutoka magharibi ya jiji la London kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya lakini Owen anaamini ratiba hiyo haitawazuia Chelsea kutwaa taji la ligi msimu ujao.

Owen amesema United watakuwa na mageuzi makubwa msimu ujao licha ya kumaliza nafasi ya sita msimu uliopita ambapo anaamini vijana hao wa kocha Jose Mourinho watatoa changamoto kubwa kwenye mbio za ubingwa.

Owen anaipa nafasi kubwa Chelsea kutwaa ubingwa lakini mkongwe huyo hakusita kuzitaja timu za Tottenham Hotspur, Liverpool na Manchester City pia kuwa miongoni mwa watakaowania taji hilo.

Akizungumza na gazeti la Daily Star, Owen alisema “Chelsea kama mabingwa watetezi bado wana nafasi kubwa ya kutwaa taji.

“Lakini kuna timu kama Liverpool, Tottenham na timu kutoka jiji la Manchester hauwezi kuzitoa katika mbio za ubingwa.

Chelsea imesajili wachezaji wanne msimu huu ambao ni Willy Caballero, Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko na Alvaro Morata huku wakimruhusu Nemanja Matic kujiunga na Man United.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *