PICHA: Mazoezi ya Stars uwanja wa Uhuru

 

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kimeendelea na mazoezi jioni ya leo kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Botwasana
Erasto Nyoni ni kati ya wachezaji muhimu wanaotegemewa kukibeba kikosi hicho ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kwenye dimba la Uhuru Septemba 2
Winga wa Difaa El Jadidi, Simon Msuva aliwasili jijini Dar asubuhi ya leo na jioni akaungana na wenzake kwenye mazoezi hayo
Nahodha Mbwana Samatta alishindwa kumaliza mazoezi hayo baada ya kupata maumivu ya mguu. Hata hivyo daktari wa timu hiyo alisema hali yake si mbaya na kesho ataendelea na mazoezi asubuhi.
Baada ya mazoezi hayo wachezaji wa Stars walipata fursa ya kupoza kiu kwa kula madafu, pichani ni Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika klabu ya Baroka FC.
Kim Paulsen (kushoto) akiteta jambo na Samatta
Stars watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho asubuhi katika uwanja huo huo wa Uhuru kabla ya kuwapisha wageni ambao wanatarajiwa kufanya mazoezi jioni
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *