Piga Ua Mourinho Atawapa Nafasi Nyota Hawa Watatu Leo

BAADA ya sare ya bao moja nyumbani dhidi ya Swansea City Jumapili iliyopita, tumaini pekee la Manchester United kushiriki michuano ya Ulaya mwakani ni kushinda kombe la Europa msimu huu.

United iliyopo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu inaifuata Celta Vigo katika pambano la kwanza la nusu fainali ya Europa litakalopigwa usiku wa leo huku mashetani hao wakiendelea ‘kuugulia’ tatizo la majeruhi kikosini mwao.

Hawa hapa ni wachezaji watatu ambao kocha Jose Mourinho anaweza kuwapa nafasi kikosini ili afanikishe lengo lake la kujiandalia mazingira mazuri kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford wiki ijayo.

1. MATTEO DARMIAN

2017-04-16T163942Z_135362382_MT1ACI14779816_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-CHE-1024x732

Baada ya mlinzi wa kushoto Luke Shaw kuumia katika pambano dhidi ya Swansea Jumampili huku ikionekana ni wazi ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Celta, nyota anayeweza kuziba pengo hilo Matteo Darmian.

Muitaliano huyu alicheza dakika zote 90 katika mtanange uliomalizika kwa suluhu dhidi ya majirani zao Manchester City juma lililopita hivyo Mourinho ataweka matumaini yake hapa akiamini ataisaidia timu kufikia malengo yake.

2. AXEL TUANZEBE

2017-01-29T174920Z_128713760_MT1ACI14741945_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-WIG

Kinda huyu mwenye miaka 19 amekuwa akiingia na kutoka kwenye kikosi cha wakubwa cha United kwa kipindi kirefu sasa lakini kuumia kwa Eric Bailly katika mchezo dhidi ya Swansea kunaweza kumpa nafasi kuwemo kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza usiku wa leo.

Axel amekuwepo United tangu akiwa na miaka minane akizitumikia timu za vijana huku mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya wakubwa ukiwa ni wa kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic Januari ambapo alitokea benchi na kuisaidia timu yake kushinda mabao 4-0.

Kuna uwezekano mkubwa ukuta wa United ukawakosa Bailly, Phil Jones na Chris Smalling huku Marcos Rojo akiwa nje hadi msimu ujao hivyo Mourinho hana namna zaidi ya kumwanzisha Tuanzebe kama mlinzi wa kati.

3. HENRIKH MKHITARYAN

2017-04-01T143834Z_134059114_MT1ACI14771901_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-WBA-1024x683

Kuna asilimia kubwa nahodha huyu wa Armenia akaanza kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa leo kama moyo wa safu ya ushambuliaji licha ya kukosa nafasi mara kwa mara.

Mkhitaryan (27) alicheza kwa dakika 10 tu za mwisho katika mchezo dhidi ya Swansea ikiwa ni ishara kwamba alikuwa akiandaliwa kwa ajili ya mchezo huu mgumu wa leo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *