Pique abubujikwa na machozi, Barcelona ikishinda bila mashabiki Camp Nou.

katika hali ya sintofahamu inayoendelea nchini Hispania baada ya wananchi wa Catalunya kudai uhuru wao na kusababisha vurugu zilizo jeruhi watu zaid ya 300, mchezo baina ya Barcelona dhidi ya Las Palmas ulilazimika kuchezwa bila mashabiki uwanjani kwa sababu za kiusalama.

Mchezo huo uliisha kwa Barcelona kupata ushindi wa mabao 3 kwa 0 mabao yaliyofungwa na Sergio Busquets na Lionel Messi aliefunga mabao mawili.Ushindi huo umeifanya Barcelona kuendelea kuongoza ligi kwa kufikisha point 21 ikishinda michezo yake yote 7 huku wapinzani wao Real Madrid wakishika nafas ya 5 kwa kufikisha alama 14.

Gerald Pique hakusita kuonyesha hisia zake baada ya kuona picha za matukio ya polisi nchini humo wakiwapiga na kuwazuia waliojitokeza kupiga kura ya kudai uhuru wa “Katalunya” siku ya jana.

“Hakukua na dalili zozote za vurugu wala uvunjifu wa amani,lakini kwa mshangao Polisi wamefanya walichokifanya”

Chama cha mpira Hispania kililazimisha kuchezwa kwa mchezo huo kama ratiba ilivyokuwa, ingawa Barcelona walitaka mchezo huo usichezwe kupisha uchaguzi huo ambao serikali ya Hispania imesema si uchaguzi halali.

Akizungumzia kulitumikia taifa la Hispania Pique ambaye ni mzaliwa wa Catalonia alisema “niko tayari kuendelea kuchezea timu hiyo ya taifa lakini kama mwalimu na uongozi ukiona mimi ni tatizo basi nitakaa pemebeni.


uwanja wa Camp Nou ukiwa mtupu wakati timu zinajiandaa.

Sergio Busquets aliefunga bao la kwanza katika mchezo dhidi ya La Palmas.[/caption]

Lionel Messi akishangilia moja kati ya mabao yake 2.[/caption]

Maelfu ya mashabiki wakiwa nje ya uwanja wa Camp Nou baada ya milango kufungwa.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *