POGBA: NILIKATAA OFA YA MADRID NIKAJIUNGA NA UNITED

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amekiri kuwa alikataa ofa ya Real Madrid kabla ya kujiunga na Mashetani hao Wekundu majira ya joto ya mwaka jana.

Pogba 24, amekulia kwenye Academy ya klabu hiyo alivunja rekodi ya usajili wa dunia aliporejea kutoka Juventus kwa ada ya pauni 89 milioni.

“Niwe muwazi, Real Madrid walinifuata lakini nilikuwa nawaza kwenda Manchester United ambayo daima ipo moyoni mwangu.

Moyo wangu umeniambia nirejea hapa sijui kwanini na sijui kitu gani kitatokea mbeleni,” alisema Pogba.

Pogba anaendelea kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mechi dhidi Arsenal Disemba 2 ambapo alikosa mchezo wa Derby ya Manchester waliopteza kwa mabao 2-1 wikiendi iliyopita.

Usiku wa leo kiungo huyo atakosa mchezo wa pili dhidi ya AFC Bournemouth mtanange utakaopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *