PRISONS YAIPIGA SIMBA MKWARA KUELEKEA MECHI YA LEO

Tanzania Prisons imeipiga mkwara mzito Simba na kujinasibu kuwa wataondoka na pointi zote tatu katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Taifa jioni ya leo.

Prisons ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 38 inahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kujiimarisha kwenye msimamo.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Avintishi Abdallah amesema wamefanya maandalizi mazuri na wachezaji wapo kwenye hali nzuri ya kiuchezaji na watapambana kuhakikisha wanashinda leo.

“Tunafahamu Simba ni timu bora kwa sasa, inaongoza ligi na ipo kwenye kiwango bora lakini leo wasitegemee mteremko tumejiandaa kuondoka na pointi zote tatu na uwezo huo tunao,” alisema Katibu huyo.

Katibu huyo alisema katika mchezo wa leo watakosa huduma ya nyota wao Laurian Mpalile na Lambert Sabianka ambao ni majeruhi.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Simba ilishinda kwa bao moja lililofungwa na John Bocco.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *