PSG kumwaga tena ‘mpunga’ kuwatibulia United, Madrid

BAADA ya kumnasa Neymar, klabu tajiri ya Paris St Germain imepanga kutoa pesa zaidi katika usajili huu safari hii ikifunga kazi kwa mshambuliaji Kinda wa As Monaco Kylian Mbappe na kiungo Fabinho

Mbappe ambaye anawaniwa na Real Madrid pia huku Fabinho akiwaniwa na Manchester United wote huenda wakajiunga na Paris St Germain kwa kiasi cha paundi 201 milioni kabla dirisha la usajili halijafungwa agosti 31

Paris St Germain wana uhakika kuwa hawatovunja sheria za FFP katika usajili hivyo wanajiandaa kutoa pesa zaidi na kuwanyakua wachezaji hao kutoka kwa mahasimu wao katika ligi kuu nchini Ufaransa

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *