PSG walianza na Ronaldo kabla ya Neymar

IMEFAHAMIKA kuwa matajiri wa jiji la Paris, PSG walilazimika kumsajili Neymar baada ya Cristiano Ronaldo kugomea ofa yao na kusisitiza anataka kubakia Real Madrid.

PSG waliushangaza ulimwengu baada ya kulipa paundi 200 milioni kama gharama za manunuzi ya mkataba kati ya Neymar na Barelona.

Baada ya taarifa kusambaa kwamba Ronaldo anataka kuondoka Madrid baada ya kupewa tuhuma za ukwepaji kodi nchini Hispania, PSG walitupa ndoano yao lakini walipoona hakuna dalili za kufanikiwa ndipo wakahamia kwa Neymar.

Licha ya ukaribu wake na Rais Nasser Al-Khelaifi wa PSG, Ronaldo aligoma kuhamia kwa wakali hao wa Ligue 1 huku ikielezwa kuwa kama nyota huyo ataamua kuondoka Madrid basi atarejea nchini Uingereza na si kwingineko.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *