PSG YAINGIA VITANI NA EVERTON KWA ROJO

Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint Germain imeingia katika vita ya kuwania saini ya mlinzi wa Manchester United, Marcos Rojo na klabu ya Everton ambayo ilionyesha nia muda mrefu.

Gazeti la the Sun, limeripoti kuwa Meneja Marco Silva anataka kumvuta raia huyo wa Argentina Goodison Park ingawa atakutana na upinzani kutoka kwa PSG, Marseille na Zenit St Petersburg.

Meneja wa United, Jose Mourinho anataka kuuza mlinzi mmoja ili kupata pesa ya kusajili beki mpya huku Rojo akionyeshwa mlango wa kutokea.

Rojo 28, alikubaliana na Mashetani hao kuongeza mkataba mrefu zaidi msimu uliopita lakini inaonekana siku zake za kuishi Old Trafford zinahesabika.

Mlinzi huyo amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara ambapo msimu uliopita hakucheza mechi nyingi.

Mbali la Rojo walinzi wengine Phil Jones na Chris Smalling wanaweza pia kuonyeshwa mlango wa kutokea msimu huu.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *