PSG YAJITOSA NAYO KWA FELLAIN

Kiungo Marouane Fellaini wa Manchester United amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na klabu mbalimbali kufuatia mkataba wake kuelekea ukingoni mwishoni mwa msimu baada ya kugoma kuongeza mwingine.

Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa akifuatiliwa na Paris Saint German kama mbadala wa Thiago Motta ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu.

Fellaini amegoma kuongeza mkataba mara mbili na United kitu ambacho kinaongeza tetesi kuwa hataonekana Old Trafford kuanzia msimu ujao.

Meneja wa United, Jose Mourinho hayuko tayari kumruhusu kiungo huyo kuondoka huku akiendekea kuwashawishi mabosi kuhakikisha wanambakisha kwa njia yoyote.

Fellain 30, alianza vizuri msimu baada ya kufunga mabao manne kati ya mwezi Agosti na Septemba kabla ya kupata majeraha ya goti yanayo msumbua hadi sasa.

PSG wameandaa kumpa mkataba wa miaka minne ambao kwa mwaka atalipwa karibia pauni 5.4 milioni kwa mwaka baada ya kukatwa kodi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *