Rais UEFA aunga mkono mabadiliko ligi kuu Uingereza

NYON, Uswis
RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) Aleksander Ceferin ameunga mkono mipango ya wadau wa ligi kuu nchini Uingereza kupunguza muda wa dirisha la usajili ili lifungwe kabla ligi haijaanza.

Jopo la klabu kubwa barani Ulaya lilituma barua pepe kwa UEFA kutoa malalamiko yao juu ya muda wa dirisha la usajili na baada ya malalamiko hayo kusikilizwa wiki hii kutakuwa na zoezi la upigaji kura juu ya maamuzi ya kupunguza muda wa usajili.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin

Ceferin aliandika “Nina taarifa ya kuwepo majadiliano Ulaya juu ya kupunguza muda wa dirisha la usajili katika majira ya joto na tumefuatilia hilo, kwa muono wangu,sio vizuri mchezaji kucheza ligi na timu hii kabla ligi haijaanza na ikianza akawa na klabu nyingine kabla dirisha halijafungwa”.

Kumekuwa mkanganyiko juu ya muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili Uingereza wakiwa wanafunga Agosti 31 huku Hispania wakifunga usiku wa Septemba mosi yote ikiwa ni baada ya ligi kuanza na hivyo kuamua kufanya mabadiliko hayo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *