RASMI YANGA YAJIENGUA KAGAME CUP

Baada ya jana kuzagaa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Yanga imejitoa kushiriki michuano ya Kagame hatimaye uongozi umethibitisha jambo hilo.

Kupitia kwa msemaji wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema ni kweli wamejitoa kushiriki michuano hiyo ili kuwapa nafasi wachezaji wao kupumzika baada ya kucheza mechi nyingi mfululizo.

Michuano hiyo imepangwa kuanza Juni 29 na Yanga ilikuwa imepangwa kundi C pamoja na timu za Simba, St. George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.

Ten amesema wamecheza mechi nyingi mfululizo hivyo wachezaji wao wamechoka na kama wangeshiriki michuano hiyo basi wasingefanya vizuri huku wakiwa na mechi ya kombe la Shirikisho Afrika mwezi ujao.

“Ni kweli hatutashiriki michuano ya Kagame na Katibu mkuu ameandika barua na kuipeleka TFF kuwaambia tumejitoa katika mashindano.

“Ukiangalia katika mechi zetu za mwisho tulicheza mechi mfululizo halafu tukashiriki tena SportPesa halafu bado Kagame kwahiyo tumewaruhusu wachezaji wetu wapumzike ili kujiandaa na mechi ya makundi kombe la Shirikisho Afrika,” alisema Ten.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *