Ronaldo AINADI tuzo yake ya BALLON D’ OR.

NYOTA wa Real Madrid,Christiano Ronaldo ameinadi tuzo yake ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’ Or aliyoishinda mwaka 2013 katika mnada uliofanyika jijini London.

Mauzo ya tuzo hiyo yatatumika kusaidia jamii kupitia mfuko uitwao “Make-A-Wish Foundation” unaotoa misaada kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wale wenye maradhi.Tuzo hiyo ilinunuliwa na Idan Ofer,tajiri mkubwa wa Jerusalem kwa kiasi cha Euro laki sita (600,000) kwa mujibu wa gazeti la Marca la nchini Hispania.

Ronaldo akionyesha moja kati ya tuzo zake za mchezaji bora wa dunia.

Jose Mourinho na Pep Guardiola ni miongoni mwa watu walioshiriki tamasha hilo kwa kuchangia kiasi cha paundi 27,000 sawa na Euro 30,000.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *