Ronaldo ndani ya Urusi, Arjen Roben akitundika daluga kimataifa.

Timu ya taifa ya Ureno hapo jana ilifanikiwa kufuzu michuano ya kombe la dunia baada ya kuipa kipigo cha mabao 2 bila majibu taifa la Switzerland katika mchezo uliopigwa jijini Lisbon.

Ureno walifungua karamu ya magoli baada Johan Djourou mlinzi wa Uswizi kujifunga katika dakika ya 4 ya mchezo huku bao la pili lililoihakikishia ushindi Ureno likifungwa na Andre Silva. Ushindi huo umeipeleka Ureno kileleni mwa kundi B ikifikisha alama 27 sawa na Uswizi lakini Ureno ikizidi kwa tofaut ya magoli 2.

Andre Silva akifunga bao la pili katika mchez huo.

Wakati Ureno wakishangilia ushindi,mabao 2 yaliyofungwa na Arjen Roben dhidi ya Sweden hayakutosha kuipeleka Uholanzi kombe la dunia,ikishika nafasi ya 3 kwa alama 19 sawa na Sweden walioizidi Uholanzi kwa idadi ya magoli.

Arjen Roben mwenye miaka 33 ametangaza kustaafu soka la kimataifa akiwa ameichezea Uholanzi mechi 96 akifunga mabao 37.Robin van Persie, Klaas Jan Huntelaar na Patrick Kluivert ndio wachezaji pekee waliofunga magoli zaidi ya hayo.

Ni vyema kuwaachia kizazi kipya,ulikua ni usiku wenye hisia kubwa kwangu, nilitambua kabla ya mchezo kwamba leo ndio mwisho wangu na haikua rahisi kwangu. Nafurahi nimeweza kucheza vizuri leo na kufunga mabao mawili na kuwaaga waholanzi kwa mchezo mzuri.

Arjen Roben nahodha wa Uholanzi alieamua kutundiga daruga kimataifa.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *