Rufaa ya Liverpool yapigwa chini

RUFAA ya Liverpool kuomba kupunguzwa kwa adhabu ya kutocheza mechi tatu aliyopewa mshambuliaji wao Sadio Mane imetupiliwa mbali na chama cha soka nchini Uingereza hivyo ataendelea na adhabu yake kama kawaida.

Mane alimkanyaga usoni kipa wa Manchester City, Ederson na kumuumiza vibaya tukio lililopelekea nyota huyo aoneshwe kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 37.

Kupigwa chini kwa rufaa hiyo kunamaanisha Mane atakosa mechi tatu zijazo za ligi kuu nchini Uingereza ingawa ataruhusiwa kucheza mechi za ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mane ataukosa mchezo wa nyumbani dhidi ya Burnley September 16, Leicester City (Carabao Cup) September 19 na mechi nyingine ya ligi kuu siku tatu baadae.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *