SAFARI YA NDEMLA YASOGEZWA MBELE, KUONDOKA ALHAMISI

Safari ya kiungo wa Simba,Said Ndemla ya kuelekea Sweden kufanya majaribio kwenye klabu ya AFC Eskilstuna itafanyika keshokutwa Alhamisi badala ya leo kama ilivyotangazwa jana.

Idara ya habari ya klabu hiyo ilitangaza jana kuwa kiungo huyo ataondoka jioni ya leo kuelekea Sweden ambapo atakaa huko kwa siku 14.

Taarifa iliyotolewa leo na Idara hiyo ilikuwa ikisomeka hivi: “Tunapenda kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele sasa atasafiri Alhamisi.

Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *