SALAH aipeleka Misri kombe la dunia.

Nyota wa Liverpool, Mohammad Salah amewapeleka mafarao (Misri) kwenye kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika miaka 28 baada ya kufunga mabao 2 dhidi ya taifa la Congo kwemye mchezo uliopigwa jijini Alexandria katika dimba la Borg El Arab.

Wakati Misri inayonolewa na Hecto Couper ikiwa ikiongoza kwa bao 1 lililofungwa na Salah,Congo almanusura waiharibu sherehe ya Mafarao baada ya kusawazisha bao kupitia kwa Arnold Bouka alieunganisha moja kwa moja mpira wa krosi uliowashinda walinzi wa Misri na kuzima kelele za jiji la Cairo lililokua limejaa bendera za taifa hilo.Ilikua katika dakika ya 95 Mohamed Salah alipofunga mkwaju wa penati na kuamsha tena nderemo katika kila kona ya mitaa nchini humo na kuwahakikishia Mafarao safari ya kwenda nchini Urusi.

Maelfu ya mashabiki wa Misri walijitokeza barabarani kushangilia ushindi huo mkubwa, uliokata ukame wa kushiriki kombe la dunia, ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki tangu kombe la dunia la mwaka 1990 nchini Italia.

Ushindi huo unaifanya Misri kuongoza kundi E kwa kufikisha alama 12 ikiipiku Uganda yenye alama 8, na kuzimisha ndoto za wana Afrika mashariki hao kushiriki kombe la dunia.

matukio zaidi katika picha .
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *