SALAMBA AAHIDI FURAHA FAINALI SPORTPESA

Mshambuliaji mpya wa timu ya Simba, Adam Salamba ameahidi kuwa watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanachukua taji la SportPesa kwa kuifunga Gor Mahia keshokutwa Jumapili.

Salamba alicheza dakika chache katika mchezo wa jana wa nusu fainali dhidi ya Kakamega lakini akionyesha uwezo mkubwa.

Simba imekwenda kushiriki michuano hiyo bila washambuliaji wake nyota Emmanuel Okwi na John Boko ambao ni majeruhi hivyo Salamba na Mohammed Rashid ambao wote wamesajiliwa hivi karibuni wana jukumu la kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Wekundu hao.

Salamba ameongeza kuwa wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na wachezaji wataingia kutimiza majukumu yao kuhakikisha wanashinda huku akiwataka mashabiki waendelee kuwaombea dua.

“Kikubwa tunawaomba mashabiki na Watanzania watuombee ili tufanikiwe kuchukua taji hili, sisi wachezaji tutatimiza majukumu yetu uwanjani,” alisema Salamba.

Kaimu kocha mkuu wa mabingwa hao, Masoud Djuma alikiri kuwa mshambuliaji huyo alifanya vizuri katika mechi yake ya kwanza licha ya kucheza dakika chache.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *