SARE YA NAMFUA YAIWEKA YANGA KILELENI KWA MUDA

Licha ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Singida United mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga imekaa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 17.

Azam FC ambayo ina pointi 16 itashuka dimbani muda mfupi ujao katika uwanja wa Azam complex kuwakabili Maafande wa Ruvu Shooting ambapo kama itashinda itafikisha alama 19 na kuwashusha Yanga kileleni.

Katika mchezo huo Singida walimiliki sehemu kubwa ya mchezo huku wakitengeneza nafasi ambazo hazikuweza kuzaa mabao.

Katika eneo la kati la uwanja Singida waliweza kuliteka ambapo viungo Mudathir Yahya, Kenny Ally na Tafadzwa Kutinyu waliweza kuwamudu Papy Tshishimbi, Pato Ngonyani na Pius Buswita hasa kipindi cha pili.

Sare hiyo ni ya tano kwa Yanga msimu huu ikiwa ni ya pili mfululizo baada ya wikiendi iliyopita kubanwa mbavu na Simba ya bao 1-1 katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa upande wa wenyeji Singida wao walikuwa wakipata sare ya tatu mfululizo wakiwa na alama zao 14.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo ni

Singida United 0-0 Yanga
Kagera Sugar 1-1 Tanzania Prisons
Njombe Mji 0-0 Mbao FC
Ndanda FC 0-0 Mtibwa Sugar

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *