SERIKALI: Tupo pamoja na TFF kufanikisha AFCON (U17)

SERIKALI imesema itakuwa bega kwa bega na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), katika kuhakikisha maandalizi kuelekea michuano ya Mataifa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanakwenda vizuri.

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa AFCON kwa vijana iliyopangwa kufanyika mwaka 2019 na tayari kamati ya ufundi imeundwa.

Kamati hiyo inaongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Yusuf Singo, katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, mkurugenzi wa ufundi TFF, Salum Madadi, Henry Tandau, Danny Msangi na Almas Kasongo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Serena, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amesema kufanikisha fainali hizo sio jambo la ghafla hivyo ni lazima maandalizi yafanyike mapeminavyotakiwa.

Mwakyembe alisema hayo wakati alipokutana na kamati hiyo kwa mara ya kwanza na kusema wakishindwa watakuwa hawana cha kuwaambia watanzania kwa sababu ni suala walilolijua muda mrefu.

“Tuliomba wenyewe mwaka 2013 kuandaa mashindano haya na 2015 tukajibiwa na kupewa nafasi hiyo, ninaamini tutafanya vizuri.,” alisema Mwakyembe.

Aidha Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Leodgar Tenga, alisema atatumia nafasi yake katika kuhamasisha maandalizi kwa kuwa anajua mahitaji yanayotakiwa ni mengi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *