SHABIKI KINDA WA SUNDERLAND AFARIKI DUNIA

MTOTO shabiki wa Sunderland, Bradley Lowery aliyekuwa akipambana na ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu amefariki dunia leo.

Kinda huyo (6) aliteka hisia za wadau wengi wa soka hasa baada ya kuwa rafiki mkubwa wa straika wa zamani wa Sunderland, Jermain Defoe ambaye alikuwa karibu nae katika kipindi chote cha kuugua kwake.

Taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Facebook wa familia ilisema mtoto huyo amefariki mchana wa leo Ijumaa akiwa mikononi mwa wazazi wake.

Bradley na Defoe walipiga picha juma lililopita nyumbani kwa kinda huyo Blackhall, County Durham, katika tafrija maalum ya kumuaga akiwa kitandani kwake.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *