SIMBA KUKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA JUMAMOSI NA RAIS MAGUFULI

Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba itakabidhiwa kombe lake la ubingwa Jumamosi Mei 19 katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuhudhudhuria mchezo wa soka tangu alipoingia madarakani Oktoba 2015.

Kabla ya kuwakabidhi Simba taji hilo la ubingwa Rais Magufuli atakabidhiwa kombe la CECAFA la vijana wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ walilotwaa nchini Burundi.

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema wamemuandikia barua Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kumuarifu Rais Magufuli kwa ajili ya kujitokeza katika hafla hiyo.

“Tunatarajia Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi wa mechi ya Simba dhidi ya Kagera na ndiye atakaye kabidhi kombe kwa mabingwa wapya Simba kama ratiba yake haitabadilika,” alisema Karia.

Rais Karia amesema kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa sh elfu tatu (3000) ili kuruhusu mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia mchezo huo.

Mchezo huo ambao utafanyika uwanja wa Taifa unatajiwa kuanza saa 8 mchana ili kutoa nafasi kwa matukio hayo kufanyika.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *