Simba kukabidhiwa ngao mpya baada kuivaa Azam

TIMU ya Simba itakabidhiwa ngao ya hisani iliyofanyiwa marekebisho ya maandishi Septemba 5 baada ya mchezo dhidi ya Azam FC utakaofanyika katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba iliifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4, Agosti 23 na kukabidhiwa ngao hiyo ambayo maandishi yake yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza yalikosewa. Maneno hayo yalisomeka ‘Community Sheild’ badala ya Community Shield.

Ngao mpya baada ya marekebisho

Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Alfred Lucas amewaambia waandishi wa habari kuwa ngao hiyo imefanyiwa marekebisho na Simba itakabidhiwa Septemba 5 baada ya mchezo dhidi ya Azam katika uwanja wa Uhuru.

“Ngao ya hisani imefanyiwa marekebisho katika maneno yaliyokuwa yamekosewa na itakabidhiwa kwa Simba baada ya mechi dhidi ya Azam Septemba 5,” alisema Lucas.

Hii sio mara ya kwanza kwa ngao ya hisani kuwa na mapungufu kwani Agosti mwaka jana Azam FC ilitwaa ngao ambayo ilibanduka maandishi pale pale uwanjani wakati nahodha John Bocco akiinyanyua juu.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *