SIMBA MAKINI WAAHIDI USHINDI DHIDI YA TIGO.

Timu ya soka ya Simba Makini inajitupa tena kiwanjani mwishoni mwa juma hili katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la JKY Park, maarufu kama kidongo chekundu siku ya Jumapili dhidi ya timu ya tiGO Tanzania majira ya saa 1 usiku.

Akizungumza na mtandao wa Simba Makini, mwalimu mkuu Erick Zomboko “Dizo One” amekiri kuridhishwa na mazingira ya kambi ya timu hiyo na huduma zote ambazo wamepewa na uongozi, zilizomfanya akamalishe majukumu yake ya kitaalamu kwa urahisi zaidi.

Tumepata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi kama timu, nimeyatolea maelekezo mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye mchezo wetu uliopita. Vijana wamejituma vya kutosha mazoezini, hivyo basi ni matumaini yangu watafanya kile ambacho tumekifanyia mazoezi kwa pamoja katika dakika 90 za mchezo wa jumapili. alisema Dizo Moja.

Naye nahodha wa timu hiyo Frank Rweyemamu, alijinasibu kuhakikisha wanawapa furaha washabiki wao kwa kucheza kandanda safi na kuibuka na ushindi mnono siku ya jumapili.

Tunateseka sana tukicheza kwenye viwanja visivyo na ubora, lakini kwa jumapili niwaahidi washabiki na wapenzi wetu hatutawaaangusha. wapinzani wetu ni timu nzuri lakini sisi tumejiandaa zaidi, ari na morali iko juu kuelekea mchezo huo. Tunachoomba ni uzima tu kufikia siku hiyo, alisema Frank Rweyemamu.

Kwa upande wao Uongozi chini ya Mwenyekiti Hussein Mlinga “Kita” amewaomba washabiki kujitokeza kwa wingi kiwanjani kushuhudia burudani “tikitaka” kutoka kwa Simba Makini.

Simba Makini inatarajiwa kumtumia mchezaji wake Hemedi Mauli “Meddy” aliekua nchini marekani kwa majaribio ya wiki mbili kwenye ligi ya MLS alierejea jana usiku akisubiria majibu yake.

Wachezaji wengine wanaotegemewa kuwepo jumapili ni pamoja na Ally Mikoi “Kisugu”, Iddi Size,Saleh Mohammed, Alpha Honest,Jurgen Sadiki “Cazorla”, Omary Hoza, Ally Lota,Issa Masoud,Samwel Mbai, Waladin Kano “Tycoon”,Richard Bebwa na Frank Gwaluma.

Simba Makini wakijaribu kutafuta goli kwenye mchezo wao dhidi ya SDF

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *