SIMBA MAKINI YAISHIKISHA ADABU CHANNEL TEN

Timu ya Simba Makini jana imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Channel Ten katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park saa 1 jioni.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi na kushambuliana kwa zamu na timu hizo zilienda mapumziko bila kufungana.

Makini walirudi kwa kasi na kupata mabao hayo matatu kupitia kwa Ramadhani Hassan,Idd Mkambala na Hemedy Mauli wakati bao la kufuatia machozi la Channel Ten likifungwa na Dulla Ozil kwa mkwaju wa penati.

Hata hivyo Simba Makini walikuwa na nafasi ya kupata mabao mengine zaidi kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza.

Ushindi huu ni kama wamelipa kisasi kwani Januari 28 mwaka huu walikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Yanga Facebook Fans.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *