SIMBA MAKINI YATOA KICHAPO ‘HEVI’ KWA TIGO

Timu ya Simba Makini imetoa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Tigo katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park.

Mchezo huo ulioanza saa moja usiku ulikuwa na upinzani huku Makini wakitawala zaidi lakini wakikosa nafasi kadhaa.

Makini walienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na Hemed Mauli na Idd Mkambala huku Tigo wakitoka patupu.

Ramadhan Hassan alipigilia msumari wa mwisho na kuhitimisha ushindi huo mnono kwa upande wa Makini.

Kabla ya mchezo huo Makini walikuwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya Mwenge katika mchezo wa nusu fainali ya Bonanza.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *