SIMBA, MO WAMALIZANA KILA KITU SAWA KUANZA KUMWAGA MANOTI

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwa mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’ amekubali kuwekeza asilimia 49 kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Mo alishinda zabuni ya kuwekeza ndani ya klabu hiyo akitaka asilimia 50 lakini Serikali iliagiza klabu yoyote inayomilikiwa na wanachama inatakiwa mwekezaji kupewa asilimia 49.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Manara amewaambia Waandishi wa habari kuwa tayari MO amekubali na kila kitu kimekaa sawa.

“Niwatoe hofu wapenzi na Wanachama wa Simba kuwa MO amekubali kuwekeza kwa asilimia 49 kama maelekezo ya Serikali ilivyoagiza,” alisema Manara.

Simba itafanya mkutano wake mkuu wa dharura Jumapili Mei 20 ukiwa na dhamira ya kubadili mfumo wa uendeshwaji kutoka umiliki wa wanachama kwenda kwenye hisa.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *