SIMBA NJOONI KWA WINGI JUMAPILI TUANDIKE HISTORIA

Wanachama wa klabu ya Simba wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu utakaofanyika siku ya Jumapili kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere kuanzia saa 2 asubuhi.

Mkutano huo utakuwa na ajenda 10 huku ile inayosubiriwa kwa hamu ikiwa ni kumtangaza mshindi wa zabuni ambaye atawekeza hisa za asilimia 50.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Hajji Manara amesema mkutano huo utaenda kuandika historia katika soka nchini ambapo itakuwa timu ya kwanza kujiendesha kwa mfumo wa hisa.

Manara amesema pia Simba itakuwa moja ya klabu kubwa Afrika ambayo itakuwa inashindania mataji kama itafanikiwa kuingia katika mfumo huo kutokana na uwekezaji utakaofanyika.

“Niwatake wanachama wa Simba kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili kwenye mkutano mkuu ili kuweza kuliendea jambo hili lenye manufaa mapana kwa klabu nakuweka historia katika soka la nchi hii,” alisema Manara.

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *