Simba Wameamua, Okwi Kutua Nchini Jumamosi

MSHAMBULIAJI kipenzi cha Wanasimba Emmanuel Okwi atatua nchini keshokutwa Jumamosi kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wekundu hao baada ya makubaliano kufanyika wiki iliyopita nchini Uganda.

Okwi amekuwa akitajwa kurejea Simba tangu alipovunja mkataba na klabu ya Sonderjyske ya Dernmark kabla ya kusaini mkataba wa muda mfupi na Sports Club Villa ambao tayari umemalizika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspope amewaambia Waandishi wa Habari kuwa mchezaji huyo atatua nchini Jumamosi na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Emmanuel Okwi

“Okwi atatua nchini Jumamosi na atasaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano nasi,” alisema Hanspope.

Mwenyekiti huyo amepinga kauli za baadhi ya mashabiki wanaosema usajili wa nyota huyo hautaisaidia Simba kwa kuwa hawezi kurudi na ubora wake aliokuwa nao miaka minne iliyopita kutokana na umri wake kuanza kumtupa mkono.

“Okwi amerejea Villa katika mechi chache za mwisho amefunga mabao saba, sasa mchezaji kama huyo unasemaje ni mbaya,” alihoji Hanspope.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *