SIMBA YABANWA MBAVU NA MWADUI KAMBARAGE

Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Simba imelezamishwa sare ya mabao 2-2 na Mwadui FC katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Matokeo hayo yamefanya Simba kuizidi pointi tano watani wao wa jadi Yanga wanao wafukuzia kwa karibu.

Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya tisa kupitia kwa John Bocco kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Shiza Kichuya.

Hata hivyo Bocco alishindwa kuendelea na mchezo kufuatia kupata maumivu ya mguu na kutolewa uwanjani dakika ya 29 nafasi yake ikachukuliwa na Laudit Mavugo.

Mshambuliaji Emmanuel Okwi alifunga bao lake la 14 msimu huu na la kwanza nje ya ardhi ya Dar es Salaam kwa mkwaju wa penati dakika ya 71 baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi Joram Mgeveke.

Nyota wa zamani wa timu ya Yanga David Luhende na Paul Nonga ndio waliofunga mabao kwa upande wa Mwadui ambayo yamepunguza kasi ya Wekundu.

Simba ilimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mlinzi Juuko Murshid kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *