Simba Yaendelea Kuusaka ‘Msumeno’ Morogoro

TIMU ya Simba ipo mjini Morogoro ikiendelea kutafuta ‘msumeno’ wa kuikatia Mbao FC katika mchezo wa fainali ya kombe la FA utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Jumamosi ijayo.

Simba ilisafiri jana kuelekea Mjini humo kuweka kambi ya muda mfupi ili kuivutia kasi Mbao kabla ya Alhamisi kuelekea Dodoma kwa ajili ya mtanange huo wa kukata na shoka.

Mratibu wa klabu hiyo Abbas Ally amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri ambapo wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wamewahakikishia ushindi katika mchezo huo huku akisema beki Hamad Juma ndiye mchezaji pekee atayekosa mchezo huo kutokana afya yake kutokuwa vizuri.

IMG-20170519-WA0012[1]

“Kikosi kipo vizuri maandalizi ya fainali yanaendelea, wachezaji wote wana morali kubwa tunategemea kuanza safari ya kuelekea Dodoma ila beki wetu Hamad Juma hakusafiri na timu kutokana na kutokuwa fiti,” alisema Abbas

Mbao kwanupande wao wameshawasili Dodoma na kuendelea na mazoezi yao wakiwa na morali baada ya kufanikiwa kusalia ligi kuu kwa kuibamiza Yanga bao 1-0 Jumamosi iliyopita.

Timu hizo zitakutana kwenye mchezo huo huku Simba ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi katika mechi mbili za ligi ambapo katika mchezo wa mwisho uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Wekundu hao walitoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda mabao 3-2.

Timu hizo zinagombea ubingwa huo ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *