SIMBA YAIFUATA AZAM FAINALI KAGAME

Timu ya Simba imeingia fainali ya michuano ya kombe la Kagame baada ya kuifunga JKU ya Zanzibar bao moja bila katika mtanange uliopigwa uwanja wa Taifa.

Simba itakutana na Azam FC siku ya Ijumaa katika uwanja huo huo wa taifa katika mchezo wa fainali.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Simba walifika zaidi langoni kwa JKU.

Meddie Kagere aliifungia Simba bao hilo dakika ya 45 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Nicholas Gyan.

Licha ya kufunga bao hilo Kagere pamoja na Mohammed Rashid waliocheza washambuliaji pacha walipoteza nafasi za wazi ambazo zingeifanya Simba kuondoka na ushindi mnono mzaidi.

Mlinda mlango Deogratius Munish ‘Dida’ alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya washambuliaji wa JKU iliyokuwa ikielekea wavuni.

JKU na Gor Mahia zitakutana katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu siku hiyo hiyo ya Ijumaa.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *