SIMBA YAIOMBA TFF KUPUNGUZA VIINGILIO MECHI YA KAGERA

Uongozi wa klabu ya Simba umeliomba Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kupunguza viingilio kutoka sh 3000 mzunguko hadi 2000 katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi.

Mchezo huo utatumika kwa Simba kukabidhiwa kombe la ubingwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli katika uwanja wa Taifa mchezo utakaoanza saa 8 mchana.

Jana Rais wa TFF, Wallace Karia alitangaza kiingilio cha chini cha mchezo huo kuwa sh 3000 lakini leo Simba imeomba kipungue zaidi ya hapo ili kuwezesha mashabiki kujitokeza kwingi kusherehekea ubingwa.

Msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara amesema kiingilio cha chini kikiwa sh 2000 kitavutia mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia wakikabidhiwa ubingwa.

“Tumeiandikia barua TFF kuiomba kushusha viingilio katika mchezo wetu ujao dhidi ya Kagera ili kuwezesha mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia tukikabidhiwa ubingwa,” alisema Manara.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *